The House of Favourite Newspapers

Chama: Mashabiki Tulieni, Tunatoboa Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika

0

LICHA ya kuanza vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakipoteza michezo yao miwili ya kwanza, kiungo mshambuliaji wa Simba, Mzambia Clatous Chama ameweka wazi kuwa anaamini kikosi chao kina nafasi ya kurekebisha makosa na kufuzu hatua ya robo fainali.

Mara baada ya michezo miwili ya kwanza ya hatua ya makundi kikosi cha Simba mpaka sasa kinabuluza mkia kwenye msimamo wa kundi C, la mashindano hayo wakiwa hawajakusanya pointi hata moja.

Kesho Jumamosi, Simba wanatarajiwa kushuka tena uwanjani kuvaana na Vipers ya Uganda katika mchezo wao wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utapigwa nchini Uganda, huku Simba wakihitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Chama alisema: “Tunafahamu tulipo na wapi tunapaswa kuwa, tunajua kwa kiasi kikubwa Wanasimba wameumizwa na matokeo ya michezo yetu miwili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Lakini bado tunaamini tuna nafasi ya kufanya vizuri na kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano haya, tuna michezo minne ambayo imebaki kufanikisha hilo na tutajitoa kucheza mechi hizo kama fainali.”

Stori na Joel Thomas

KUMEKUCHA! WAARABU WAIBEBA YANGA MALI, SIMBA IWE ISIWE VIPERS ANAKUFA KWAO | KROSI DONGO

Leave A Reply