The House of Favourite Newspapers

CHAMPIONI, SPOTI XTRA, GLOBAL TV NDANI YA VIUNGA VYA EVERTON

Saleh akiwa na Zouma.

TUNAPAA tu! Hivi ndivo unavyoweza kusema baada ya Timu ya Global TV Online, Magazeti la Championi na Spoti Xtra yanayochapishwa na Global Publishers kutua katika viunga vya Timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza, Everton na kufanya mazungumzo maalum na wachezaji wake pamoja na meneja wao, Mreno, Marco Alexandre Saraiva da Silva.

Salh akiwa na kocha Silva.

Kupitia kwa Mhariri wake Mkuu, Saleh Ally, Championi, Spoti Xtra na Global TV yametia kambi nchini Uingereza tangu mwanzoni mwa wiki hii ambapo tulishuhudia michezo ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kati ya Liverpool na Porto ambao Liverpool aliibuka na ushindi wa bao 2-0, na baadaye kati ya Manchester United na Barclona pale Old Trafford ambapo Man U alichapwa bao 1-0.

Saleh akiwa na Jagielka.

Safari yetu haikuishia hapo tu, iliendelea mpaka makao makuu ya Everton tukiongozwa na kampuni ya SportPesa wanayoidhamini Everton ambapo tumefanya mahonjiano na beki wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, ambaye kwa sasa anakipiga Everton kwa mkopo, Kurt Zouma, Meneja wa Everton, Marco Silva na kapteni wa timu hiyo, Phil Jagielka.

Usikose gazeti la Championi Jumamosi kesho na Spoti Xtra Jumapili pamoja na Global TV Online kusikia walichokizungumza Jagielka, Zouma na kocha wao, Championi itabaki kuwa juu, SpotiXtra itabaki kileleni!

Comments are closed.