The House of Favourite Newspapers

Changamkia Magazeti ya Global Ushinde Mjengo Huu

0

NYUMBA (1)Muonekano wa mjengo huo kwa nje ukiwa katika hatua za mwisho za matengenezo.NYUMBA (3)…upande wa mbele.NYUMBA (4)…maliwatoni.NYUMBA (5)…sebuleni.NYUMBA (7) NYUMBA (8)…koridoni.NYUMBA (9) NYUMBA (10) NYUMBA (12) NYUMBA (13)Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye shati jeupe) akijadili jambo na fundi anayemalizia matengenezo ya nyumba hiyo (aliye kifua wazi) pamoja na mfanyakazi wa Global, Deogratias..NYUMBA (14)Mrisho akikagua matengenezo ya mwisho sambamba na mandhari ya nyumba hiyo.NYUMBA (16) NYUMBA (17)

Na Mwandishi Wetu

MENEJA Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho ametembelea nyumba atakayokabidhiwa mshindi wa shindano la Shinda Nyumba, iliyopo Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.

Ziara hiyo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuangalia matengenezo ya mwisho kabla shindano hilo halijachezwa na mshindi kupatikana.

“Nyumba imekamilika kwa asilimia 99 kama unavyoona, kilichopo hapa ni vitu vidogovidogo tu vya mwisho ambavyo vitakamilika ndani ya wakati na mshindi ataipata ikiwa imekamilika kama tulivyoahidi,” amesema Mrisho.

Nyumba hiyo iliyojengwa eneo la Salasala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, ina thamani ya shilingi milioni 60 na itatolewa kwa mshindi wakati wa droo kubwa itakayochezeshwa Juni 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa meneja Mrisho, nyumba hiyo ina chumba chenye kila kitu ndani (Master Bedroom), vyumba viwili vya kulala, chumba cha chakula (Dining room), chumba cha kupumzika (Sitting room), jiko, stoo na uwanja wa kutosha nje ya nyumba.

shinda-nyumba

Leave A Reply