The House of Favourite Newspapers

Chanjo ya Rotavirus Yawekwa Kwenye Mipango ya Kitaifa Nigeria

0
Chanjo nchini Nigeria

NIGERIA imeongeza chanjo ya Rotavirus katika mpango wake wa kitaifa wiki hii ambao unatarajiwa kupunguza vifo 50,000 kutokana na ugongwa wa kuhara kwa Watoto wa mwaka, uzinduzi huo uakuja kukiwa na uhaba wa chanjo hiyo kwa mataifa mbali mbali kama Cameroon, Kenya, Senegal na Tanzania.

 

Uzinduzi huo Jumatatu ulikwenda sambamba na ukumbusho wa Wiki ya Chanjo Afrika, Maafisa kutoka Shirika la Afya Duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, pamoja na Wizara ya Afya ya Nigeria, walihudhuria uzinduzi huo katika mji mkuu Abuja.

Rotavirus

Wakati wa hafla hiyo, watoto wengi wachanga walipokea chanjo hiyo bure, huku viongozi wakiwataka raia kukumbatia kipimo hicho. Faisal Shuaib, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo ya Afya ya Msingi alisema. “Tunahitaji kutumia fursa hii wakina mama, walezi  ili watoto wetu walindwe kutokana na virusi hivi.”

 

Moses Njoku, mtafiti katika Taasisi ya Kitaifa ya utafiti na maendeleo ya madawa ya Nigeria, alisema upungufu haufai kuwa changamoto kwa Nigeria, Njoku alisema. “Nigeria inaanza kuona hitaji la kuanza juhudi za asili kuanza utafiti na uzalishaji, utengenezaji wa chanjo, pamoja na utengenezaji wa chanjo zinazojulikana.”

 

Leave A Reply