The House of Favourite Newspapers

KMC wajipanga kwa mbwembwe za hatari kuikabili Simba, Kujipima kwa Mechi za Kimataifa

0
Benchi la Ufundi la KMC

TIMU ya KMC ikijua itakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Simba imerejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo itakayopigwa septemba 7 mwaka huu.

 

KMC ilikuwa jijini Arusha kwa ajili ya mechi mbili ambapo ilikuwa inacheza na polisi Tanzania pamoja na Coastal Union ambapo imeibuka ikiwa na pointi moja baada ya kuteleza na kupoteza mchezo wa kwanza katika mechi hizo mbili.

Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi

Akizungumzia kuhusu maandalizi yao Afisa habari wa KMC Christina Mwangala amesema kuwa:

 

“Timu ilirejea Dar es Salaam siku ya jumatatu na kutoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji ambapo siku ya jumanne iliingia kambini ili kuanza mazoezi ambapo ilianza kwa program ya gym na leo asubuhi itaendelea na mazoezi ya kawaida uwanjani”

Simba ipo katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kiushinda michezo yake yote miwili

Kiongozi huyo pia amesema kuwa katika kipindi cha mapumziko timu hiyo itakuwa na program mbalimbali ikiwemo kucheza mechi za kirafiki ambapo siku ya kesho itacheza dhidi ya timu ya ugenini ya As Arta Solar 7 kutoka nchini Djibout katika uwanja wa uhuru jjijini Dar es Salaam, aliongezea kwa kusema kuwa katika kipindi hiki timu hiyo itahitaji mechi nyingi za kirafiki ili kujiandaa na mechi zijazo.

 

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply