The House of Favourite Newspapers

Chanongo, Ubwa wakaribia kuula Mazembe

0

Omary Mdose,Dar es Salaam

WATANZANIA Harun Chanongo na Abuu Ubwa, kesho Jumanne wanatarajia kurejea nchini kutoka DR Congo walipokwenda kufanya majaribio ya siku kumi katika timu ya TP Mazembe, huku dalili za kuula kikosini hapo zikiwa wazi.

Wachezaji hao kutoka katika kikosi cha Stand United ya Shinyanga, waliondoka nchini Januari 2, mwaka huu pamoja na Mkurugenzi wa Michezo wa TP Mazembe, Frederic Kitenge.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ubwa alisema wanatarajia kurejea nchini kesho Jumanne, lakini katika siku walizokuwa wakifanya majaribio, mashabiki na wachezaji wenzao walikuwa wakiwasifia kutokana na uwezo waliokuwa wakiuonyesha.

“Jumanne (kesho) tunatarajia kurejea nyumbani, mpaka sasa hatujui kama watatuchukua au la, lakini mashabiki na wachezaji wa Mazembe wamekuwa wakitusifia sana, wanasema tunaweza kuichezea timu yao.

“Wao wanasema hivyo, lakini viongozi wa timu ndiyo wana kauli ya mwisho, sasa kilichobaki ni kusubiri majibu kutoka kwa viongozi kutokana na kocha alivyotuona,” alisema Ubwa.

Inaelezwa kuwa, Chanongo na Ubwa wanatajwa kwenda Mazembe kuangaliwa uwezekano wa kuziba nafasi za Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wapo njiani kuelekea barani Ulaya kucheza soka la kulipwa.

Leave A Reply