The House of Favourite Newspapers

Charles Matondane Ateuliwa Kuwa Meneja Mpya Wa Bolt Nchini Tanzania

0

Dar es Salaam, Juni 2023: Kampuni ya usafiri kwa njia ya Taxi-mtandao barani Afrika Bolt, imetangaza uteuzi wa Charles Matondane kama Meneja Mkazi kwa shughuli zake za Tanzania. Akiwa na zaidi ya miaka 17 ya mafanikio ya ajabu katika shughuli za teknolojia barani Afrika na Ulaya, Charles ataleta uzoefu mwingi na rekodi ya mafanikio katika jukumu lake jipya.

Kwenye taaluma yake, Charles amefanyakazi na mashirika makubwa ya kimataifa kama vile Vodacom, Tigo, Velti Plc. (Ugiriki), Kirusa Inc. (Marekani), na Apollo Group (Kenya). Utaalamu wake upo katika kujenga suluhu zakisasa na kutengeneza timu zenye matokeo chanya katika nchi 15 za Afrika kwenye sekta zikiwemo Telecom, Vyombo vya Habari, Bima, Pesa kwa Simu na Huduma za Malipo.

Lengo lake kuu limekuwa katika kuendesha mabadiliko ya kidijitali na kuongoza maendeleo ya shughuli mpya ndani ya mazingira yanayolenga kibiashara.

Charles anashauku isiyoyumba ya uchanganuzi wa data na maarifa, ambayo humruhusu kutengeneza kimkakati masuluhisho ya ufanisi yenye athari chanya kwa masoko yanayoibukia, hasa Afrika. Kwa kutanguliza ubora na ufanisi katika utendaji kazi na utekelezaji wa teknolojia, mara kwa mara anatoa thamani ya kipekee kwa wateja na wadau wakuu.

“Bolt inafuraha kubwa kumkaribisha Charles kwenye timu yetu, uzoefu wake mkubwa katika nyanja ya teknolojia, pamoja na ufahamu wake wa kina wa mandhari ya Afrika, unamfanya kuwa nyongeza ya thamani katika shirika letu.

Tuna imani kwamba michango yake itaimarisha zaidi msimamo wetu, kama kiongozi katika tasnia ya usafiri kwanjia ya mtandao.” Alisema Takura Malaba, Menejawa Kanda, Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Charles amekuwa mtu mwenye ushawishi katika mabaraza mengi ya kimataifa, akionyesha utaalamu wake na uongozi wa mawazo. Alishiriki katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia kuhusu Afrika, akijihusisha kikamilifu katika mazungumzo muhimu yanayohusu Mabadiliko ya Biashara na Teknolojia barani Afrika.

Zaidi ya hayo, aliwahi kuwa mzungumzaji mashuhuri katikaUmojawaMataifawa ITU Telecom World, pamoja na GSMA World Congress 2014, ambapo alishirikisha maarifa yake kuhusu Teknolojia na Ubunifu unaochanua katika Afrika.

Akizungumza kuhusu uteuzi wake, Charles alisema: “Nimefurahi kujiunga na Bolt kwa kuchangia uzoefu wangu mkubwa katika uendeshaji wa Teknolojia ili kuleta mapinduzi katika tasnia ya huduma ya usafiri ya taxi mtandao nchini Tanzania.

Kwa kuzingatia mabadiliko ya kidijitali na masoko yanayoibuka, ninafuraha kuendeleza ufanisi na kuunda suluhu zenye matokeo kwa wateja na washikadau wa Bolt.”

Charles ana Shahada ya Kwanza katika Biashara na IT, pamoja na Diploma yaUzamili katika Sayansi ya Data na Uchanganuzi wa Biashara. Zaidi ya hayo, amepata Cheti maarufu cha Chartered Financial Analyst Level One kutoka kwa Taasisi ya CFA.

Akiwa na sifa za kipekee na ujuzi wa kina watasnia, Bolt iko tayari kuimarisha nafasi yake kama mtangulizi katika sekta ya teknolojia, akiendesha uvumbuzi na ufanisi katika tasnia ya usafirishaji. Uteuzi huu unaimarisha dhamira ya Bolt ya ubora na harakati zake za kupeana uzoefu usio na kifani wa wateja. 

Kuhusu Bolt:

Bolt ni programu bora zaidi yenye wateja zaidi ya milioni 100 katika zaidi ya nchi 45 na miji 500 kote Ulaya na Afrika. Hapa nchini Bolt ipo mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza. Tunatoa huduma ya usafirishaji wa bidhaa na mahitaji tofauti:

Usafirikiwa Taxi mtandao

Bolt Business

Bolt press kit: http://bit.ly/bolt-media-kit

Leave A Reply