The House of Favourite Newspapers

Charles Mkwasa: Hatujatoka Kwenye Mbio za Ubingwa

0
Charles Boniface Mkwasa

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa bado ni mapema kuitoa Yanga katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

 

Mkwasa ameeleza kuwa Yanga bado wanayo nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu kwa kuwa timu hiyo bado ina mechi nyingi za kucheza licha ya kuwa wameachwa kwa pointi nyingi na vinara, Simba.

Yanga imesaliwa na mechi 17 kumaliza msimu huu wa ligi, hivi sasa ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 40. Vinara Simba wana pointi 59.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mkwasa alisema: “Hatuwezi kujitoa katika mbio za ubingwa kwa sasa kwa kuwa bado tuna michezo mingi ya kucheza, tunachotakiwa kufanya ni kuwekeza nguvu katika mapungufu machache ambayo yameshajitokeza katika michezo ya hivi karibuni, ligi bado mbichi hatuwezi kusema kuwa tayari tumeuacha ubingwa.

Leave A Reply