The House of Favourite Newspapers

CHEGE: KUNA VICHWA 14 KWENYE ALBAMU YANGU

0
Chege Chigunda ‘Mtoto Wa Mama Said’

MSANII wa muziki nchini, Chege Chigunda ‘Mtoto wa Mama Saidi’, amefunguka juu ya ujio wa albamu yake mpya aliyoiachia hivi karibuni ambayo amefanya mapinduzi makubwa. Pia kafunguka kwamba albamu hiyo amewashirikisha wasanii kutoka nje ambao ni Runtown wa Nigeria na Uhuru wa South Afrika.

Chege amedondosha albamu hiyo aliyoipa jina la Runtown ambayo ina ngoma 14 na amewashirikisha wasanii 13 waliomo kwenye hiyo albamu.

Rapa Kutoka Nigeria, Runtown

Akizungumza kuhusu albamu hiyo alisema: “Kwenye albamu hiyo kuna vichwa kama Mh Temba mshikaji wangu kutoka TMK, Chid Benz, Bill Nass, Ray C, Malaika, mkali kutoka Nigeria Runtown, Uhuru kutoka South Afrika, Nandy, Dija, Sanapei na Gift.”

Chege ameshirikisha wakali 13 kwenye albamu hiyo na ngoma ya 14 ameifanya yeye mwenyewe, pia katika nyimbo hizo kuna nyimbo zingine tayari zina video.

NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Leave A Reply