The House of Favourite Newspapers

CHEMICAL AWACHANA WANAOMDISS KUVAA GAUNI


RAPA anayekimbiza kunako muziki wa Hip Hop Bongo, Claudia Lubao ‘Chemical’ amewachana wanaomdiss kuonekana amevaa gauni kuwa wakumbuke yeye ni mtoto wa kike na ana haki ya kuvaa vazi hilo.

 

Akichonga na Over Ze Weekend, Chemical aliyekuwa amevaa kigauni hicho na kutokelezea kwenye ukurasa wake wa Instagram alisema kuwa, haoni kama ni tatizo kuvaa nguo hizo japokuwa wengi wameshazoea kumuona akiwa katika mavazi ya kiume mara kwa mara.

 

“Wengi walishazoea kuniona na nguo za kiume muda wote, wakati ninavaa lile gauni nilijua tu kwamba wataiongelea kwa sababu kuongea ni kawaida yao, kwa hiyo hawaniumizi kichwa, ninachojua mimi ni mtoto wa kike hivyo nina uamuzi wa kuvaa nguo yoyote ninayoona kwangu inafaa ilimradi tu nisivunje maadili yetu ya Kitanzania,” alisema Chemical.

MEMORISE RICHARD

Comments are closed.