IKIWA ni wiki moja baada ya kuzinduliwa kwa Chemshabongo na Gazeti la Ijumaa ambap msomaji wa gazeti hilo hujibu maswali kwa ufasaha kupitia ukurasa wa pili ndani ya gazeti hilo, leo wasomaji wameanza kujinyakulia zawadi hizo nono kutoka Gazeti hilo.
Timu ya Masoko na Usambazaji ya Global Publishers ilikuwa mtaani ikimwaga zawadi hizo zikiwemo fulana huku wasomaji wengine wakirudishiwa kiasi cha pesa walichonunulia gazeti hilo katika maeneo ya Mabibo, Manzese na Mburahati jijini Dar es Salaam ambako kote ilikopita imeweza kuwazawadia zawadi wasomaji hao waliokutwa wakilisoma gazeti hilo.
Aidha, msomaji anachotakiwa ili kujinyakulia fedha Taslimu Tsh. 30,00 au fulana nikununua gazeti la Ijumaa kisha kujibu kwa ufasaha swali la chemshabongo iliyopo kwenye ukurasa wa pili na kutuma kwa namba ya maalum iliyopo kwenye ukurasa huo.
Baada ya kuhamishia mitandaoni pekee magazeti mengine ya Udaku ya Global Publishers, Ijumaa ndiyo Gazeti pekee la Burudani nchini Tanzania linalopatikana mtaani kwa sasa ambalo limeboreshwa kuanzia stori, upambaji wa kurasa, makala, machombezo na hadithi za mtunzi mahiri, Eric Shigongo.
Pia kuna kolamu zote kali zilizokuwa kwenye magazeti mengine Udaku ili kukufanya usi-miss kitu hata kimoja cha udaku iwe ndani ama nje ya Tanzania.