The House of Favourite Newspapers

Simba Yaitegea Mtego Al Ahly Dar

0

UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa umejipanga kikamilifu kuhakikisha unafanikiwa kuvuna pointi tatu katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Al Ahly.

 

Simba inatarajia kuvaana na Al Ahly, Februari 23 jijini Dar ikiwa ni mchezo wa pili wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichakaza AS Vita ya DR Congo bao 1-0 nyumbani kwao.

 

Katibu wa Simba, Dk Arnold Kashembe amesema kuwa, mipango yao yote juu ya mechi dhidi ya Al Ahly inakwenda kama ilivyopangwa, kila kitu kipo vizuri.

 

“Maandalizi yetu katika mechi yetu dhidi ya Al Ahly yanakwenda vizuri kama tulivyopanga kuhakikisha tunafanikiwa kushinda hapa nyumbani ambapo ndiyo lengo letu kubwa, kila kitu kinakwenda vizuri, hakuna shida, tunawasubiria wapinzani wetu wakati wowote wanaweza kutua.

 

“Kwa sasa tunaangalia zaidi mchezo wetu wa ligi dhidi ya Biashara tuweze kushinda kisha akili zote zitaelekea katika mchezo huo ambao ni muhimu kwetu kuweza kushinda na kusonga mbele,” alisema Kashembe.

 

Simba ipo nafasi ya pili katika kundi lake A la Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na pointi tatu na bao moja huku Al Ahly inayoongoza ikiwa na pointi 3 na mabao 3 mkononi iliyowafunga Al Merrikh, wanaoshikilia mkia katika kundi lao.

 

Al Ahly kutua kesho DarMkurugenzi wa ufundi wa Klabu ya Al Ahly, Sayed Abdelhafiz amesema wanatarajia kuanza safari ya kuja Tanzania kucheza na Simba, leo Ijumaa na kutua kesho Jumamosi lakini amesisitiza wanakuja nchini kwa lengo la kuchukua pointi tatu dhidi ya wapinzani wao.

 

Akizungumza na mtandao wa timu hiyo, Sayed alisema: “Haikuwa mechi rahisi dhidi ya Al Merrikh lakini tumepata ushindi, tuna furaha juu ya hilo, sasa tunajiandaa na safari ya kuelekea Tanzania siku ya Ijumaa kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Simba.

 

“Simba ni timu kubwa na wanacheza soka zuri la kuvutia lakini matumaini yetu tutakuwa na mchezo wenye matokeo mazuri ambao utatuwezesha kurejea Cairo na pointi tatu,” alisema Sayed.

Stori: Khadija MngwaiNa Ibrahim Mussa

Leave A Reply