The House of Favourite Newspapers

Chid Benz: Bongo Fleva Inakwenda Mbali

MSANII wa Muziki wa Ki­zazi Kipya, Bongo Fleva, Rashid Mak­wilo ‘Chid Benz’, amesema kuwa muziki huo kwa sasa unaonekana utafika mbali zaidi kutokana na jinsi wasanii wa­navyojituma kila kukicha to­fauti na zamani.

Chid ambaye amewahi kuwika na nyimbo kibao zikiwemo Dar es Salaam Stand Up, Mmeni­soma, Naitwa Nani aliomshirikisha K-Lyin na Hasira za Nini, amesema kuwa, muziki wa Bongo Fleva una­piga hatua siku hadi siku kutokana na wasanii wanavyojituma, hivyo utafika mbali zaidi.

“Muziki wa Bongo Fleva un­aweza kufika mbali zaidi kwa kuwa wasanii wanaonekana kujituma zaidi, kila siku ki­nakuja kitu kipya, wanaonye­sha uwezo mzuri wa kuhitaji kufika mbali,” alisema Chid Benz alipozun­gumza na Kilinge juzi Jumamosi.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam.

Comments are closed.