The House of Favourite Newspapers

Chilunda wa Azam FC Asajiliwa Hispania

MWANASOKA chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Shaaban Iddi Chilunda ametambulishwa rasmi Klabu ya CD Tenerife ya nchini Hispania kuwa mchezaji wao mpya kuanzia sasa baada ya kukamilisha usajili wa kuitumikia klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa akiitumikia Azam FC amesajiliwa na Tenerife inayoshiriki Segunda Division (Ligi Daraja la Kwanza) nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili.

Chilunda (20) anakumbukwa zaidi baada ya siku za hivi karibuni kutupia jumla ya mabao manne peke yake kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda na kuweka rekodi kwenye soka la Afrika Mashariki.

Chilunda anakuwa mchezaji wa pili wa Tanzania kusajiliwa na Tenerife kutoka Azam FC ya jijini Dar es Salaam baada ya Farid Musa.SIMBA DAY: CHID BENZ Afunguka Baada ya Shoo

Comments are closed.