The House of Favourite Newspapers

China, Tanzania Zaendesha Kongamano La Utamaduni Na Umuhimu Wa Mitandao

Balozi wa China nchini, Gao Wei, akiongea wakati wa kongamano hilo.

KAMPUNI ya China Federation of Internet Oktoba 28, 2019 kwa ushirikiano na Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes zimeendesha Kongamano la utamaduni na umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii (China – Tanzania Cyber Cultural Exchange) katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo limefunguliwa na Balozi wa China nchini, Gao Wei, ambaye amesema historia ya china na Tanzania ni ndefu sana na wanaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, kiteknolojia, kimichezo.

Mchekeshaji maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Anastazia Exavery maarufu kama Ebitoke.

Akiongea Katibu Mkuu wa mtandao China Federation of Internet, Zhao Hui, amesema amevutiwa na kasi ya watanzania kutumia mitandao ya kijamii ambayo inachangia kuwaleta watu pamoja.

 

Pia amesema mitandao ya kijamii sasa imefungua mlango mpya kuwa chombo kingine cha habari kufanya watu waweze kutuma ujumbe mfupi wa maandishi bure kubadilishana picha na habari mbalimbali kupitia mitandao hii ya kijamii.

Kwa upande wa wasanii waliokuwepo katika kongamano hilo ni wachekeshaji maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Anastazia Exavery maarufu kama Ebitoke na Maya Kidoti ambao wote walifunguka kujulikana kupitia mitandao ya kijamii.

Katika kongamano hilo kampuni ya Freme waliendesha droo kwa washiriki wa mkutano huo na kupata washindi kumi ambao waliwapa zawadi ya Headphone.

(STORI NA NICOLAUS TRAC – GLOBAL DIGITAL)

Comments are closed.