The House of Favourite Newspapers

CHINA YAIPA BURUNDI BONGE LA IKULU, NI JIPYAA!

Balozi wa China nchini Burundi, Li Changlin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Ezechiel Nibigira wamesaini hati ya makabidhiano ya Jengo la Ikulu ya Burundi lililojengwa kwa msaada wa China.

 

Akiongea kwenye hafla ya kusaini hati ya makabidhiano kwenye Ikulu mpya kwenye eneo la Mutimbuzi, kaskazini mwa Bujumbura, Changlin amesema makabidhiano hayo ni alama ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Burundi, na kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaweka mkazo katika kuboresha maisha ya wananchi wa Burundi na mazingira ya kazi ya watumishi wa umma wa Burundi.

 

Kwa upande wake, Nibigira ameishukuru China kwa kujenga Ikulu hiyo, ambayo Burundi haijawahi kuwa nayo tangu ijipatie uhuru mwaka 1962, na kusema kwamba hii ni mara ya kwanza katika historia kwa Burundi kupata miundombinu mizuri, na imethibitisha uhusiano imara wa kisiasa na kidiplomasia uliopo kati ya Burundi na China.

“GODZILLA Nilikuwa Nalala Nae Kitanda Kimoja, Nimeamua Kusema” – BELLA

Comments are closed.