The House of Favourite Newspapers

Chirwa atuma salamu Yanga

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Obrey Chirwa, ameweka wazi mikakati yake kuhusiana na mechi ya Jumatatu ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

 

Azam FC itapambana na Yanga katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambao utakuwa ni wa kwanza wa ligi hiyo kuzikutanisha timu hizo msimu huu.

 

Chirwa ameliambia Championi Jumamosi kuwa, mikakati yake aliyojiwekea kuhusiana na mechi hiyo ni kuhakikisha anaifunga Yanga.

 

Alisema atafurahi zaidi kama atafanikiwa kuifunga Yanga ambayo ilikuwa timu yake ya zamani katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Alisema furaha aliyoipata katika michuano ya Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar ambapo aliifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Azam iliupata ilikuwa ni ya kawaida kwa sababu alikifunga kikosi cha pili kilichokuwa na mchanganyiko wa wakongwe kidogo.

 

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu dhidi ya Yanga ambayo ni timu yangu ya zamani niliyokuwa nikiipenda. “Lakini ikitokea hiyo Jumatatu nikaifunga Yanga nitafurahi sana kwani nitakuwa nimetimiza moja kati ya ndoto zangu ambazo nimekuwa nikiziota kila siku,” alisema Chirwa.

Comments are closed.