The House of Favourite Newspapers

Chirwa Karudi Kuwafunga Njombe Mji

0
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa.

YANGA sasa imekamilika kwani kesho Jumapili mshambuliaji wake, Obrey Chirwa anatarajiwa kuanza kucheza dhidi ya Njombe Mji na imethibitishwa yupo fiti kufanya kazi yake.

Chirwa raia Zambia hakuichezea Yanga mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kesho Jumapili, Yanga itacheza na Njombe Mji mechi ya pili ya ligi hiyo kwenye Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe na Chirwa anatarajiwa kucheza kwani amepona majeraha ya mguu.

Akizungumza na Championi Jumamosi kutoka Njombe, Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh alisema; “Wachezaji wote wapo vizuri akiwemo Chirwa ambaye tunatarajia ataanza kwani yupo fiti lakini kocha ataamua.

“Kikosi chetu kipo vizuri kuelekea mchezo huo, kuhusu afya ya Chirwa yupo vizuri na kama mambo yakienda vizuri anaweza kuanza na kufanya kazi yake kama kawaida.”

Hafidh alisema Amissi Tambwe, Buruhan Akilimali na Beno Kakolanya wao wameachwa jijini Dar es Salaam kwani ni majeruhi lakini watajiunga na wenzao watakaporejea.

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Kumbuka kuwa ili kujiunga na kubashiri ili kuvuna fedha unatakiwa kutembelea tovuti ya www.sokabet.co.tz ambapo humo ndani una nafasi ya kushinda hadi shilingi milioni 100 kwa kuweka Sh 1,000 tu.

Leave A Reply