The House of Favourite Newspapers

Chombo cha anga cha Israel chaanguka mwezini

BERESHEET,  chombo cha anga cha Israel kilichorushwa Februari 22 kutoka Cape Canaveral, Florida, Marekani, kilitumia majuma kadhaa kufika mahali palipokusudiwa na baadaye kuanguka kutokana na tatizo la kiufundi.

Safari yake ilikuwa ndefu ya kupita kwenye mzunguko wa anga la dunia (orbit), kabla ya kupatwa na nguvu ya uvutano ya mwezi na kufika  huko Aprili 4.

Lengo la safari hiyo ilikuwa kupiga picha na kufanya majaribio kadhaa.

 

Umbali kwa wastani mpaka kufika mwezini ni kilometa 380,000 na Beresheet kilisafiri zaidi ya mara 15 ya umbali huo.

Mashirika ya utafiti wa anga za juu ya Urusi  (wakati wa utawala wa Kisovieti), Marekani na China pekee  yalifanikiwa kutua salama kwenye mwezi.

Israeli ilikuwa na matumaini ya kuwa nchi ya nne kufanya hivyo.

”Hatukufanikiwa lakini hakika tulijaribu,” alisema mwanzilishi wa mradi, Meja Backer Morris Kahn.

”Ninafikiri kuwa mafanikio ya kufikia tulipofika ni mazuri sana,  Nafikiri tunaweza kujivunia,” aliongeza.

Waziri Mkuu  wa Israel, Benjamin Netanyahu, akifuatilia mwenendo wa chombo hicho karibu na Tel Aviv, alisema: ”Kama mwanzo hukufanikiwa, unajaribu tena.”

Baada ya safari ya wiki saba kuelekea kwenye mwezi, chombo hicho ambacho hakikuwa na abiria kilifika kwenye eneo la mvutano wa orbit umbali wa kilometa 15 kutoka kwenye uso wa mwezi.

Mradi huo umegharimu Paundi milioni 70.

Chanzo: BBC SWAHILI

Comments are closed.