The House of Favourite Newspapers

Chomoka Na Gari Mpya Na Championi Yatikisa Dodoma

0

HII inaitwa kanyaga twende, baada ya bahati nasibu ya Chomoka na Gari Mpya na Championi, kuendelea kupepea katika mikoa mbalimbali na sasa imetinga makao makuu ya nchi, Dodoma Machi 22, 2020.

 

Ndiyo, habari imefika hadi kwenye mashamba ya mizabibu, ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa Jiji hilo wanayo taarifa kuwa kuna gari mpya aina ya Toyota FunCargo, ipo mahali na inapatikana kwa shilingi 800 tu.

Tuelewane kidogo, ukitoa shilingi 800 ukanunua gazeti la Championi, halafu kisha ukakata, kuijaza na kuituma mahali usika kuponi iliyopo kweye ukurasa wa pili wa gazeti hilo.

 

Utakuwa umeingia moja kwa moja kwenye droo ya bahati nasibu ya kushinda gari hiyo, ambayo inaendeshwa na kampuni ya Global Publishers.

 

Lakini mbali na hilo, watu 10, watakuwa wanaondoka na simu mpya kila wiki. Yaani ukitoa 1000, inarudi 200 ya kula mhindi wa kuchoma wa 100 na maji ya kandoro ya 100, lakini bado unaweza ukawa baba mwenye gari mjini.

Kila kitu kinawezekana kwani tayari baadhi ya wakazi wa Dodoma wameshaingia kwenye droo ya kwanza ya kujinyakulia simu, Smart Kitochi ambazo ni mpya kabisa.Droo ambayo inachezeshwa leo Jumatano katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar.

Balozi wa Championi kutoka Dodoma, Shafii Msangi, ndiye aliyesimamia shoo yote, wikiendi iliyopita ambapo aliikanyaga mitaa yote mikubwa ambayo inapatikana katikati ya Jiji hilo.

 

Ambapo alianza kukiwasha akiwa na gari yake ya matangazo pamoja na wacheza shoo, kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi jua lilipoiaga ardhi.

 

Akakunja jamvi na kurudi ofisini, huku akiwa ameuza magazeti kibao na kuwapa nafasi ya wasomaji kushiriki bahati nasibu hii ya kijanja kabisa.

Msangi alisema: “ilikuwa ni mwendo wa kuuza magazeti ili watu wajaze kuponi, muitikuo ulikuwa mkubwa na wenye mafaniko, nilianza kazi saa 5: asubuhi hadi saa 11 jioni.

 

“Hapo nikiwa tayari nimeshaivuruga mitaa yote mikubwa, kuanzia nanenane, kisasa, mjini kati, soko kuu, barabra ya sita, barabara ya nne,nikapanda hadi barabara ya saba na 10, uwanja wa Jamhuri, Mkuhungu, Area C, barabara ya Arusha, kisha nikaenda kukita kambi mitaa ya Msalato Mnadani.

 

“Hapo Mnadani nilitumia muda mwingi sana, kwa sababu kulikuwa na watu wengi wenye kuhitaji magazeti na kweli kazi ilikuwa nzuri sana, hadi nafunga kazi kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao walinunua magazeti na kujaza kuponi,” alimaliza Shafii.

 

Hiyo ndiyo hali halisi, kwani baada ya kuitembelea Mwanza, Arusha na Mbeya, kambi ipo Dodoma na ikikata kamba hapo inakuja mkoani kwako, kaa tayari kuipokea.

 

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua Gazeti la Championi, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

 

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Stori na Issa Liponda |GPL, Picha na Johnson Jumbe

GLOBAL HABARI MACHI 22: 1: IDADI YA WAGONJWA WA CORONA TANZANIA YAONGEZEKA..

 

Leave A Reply