The House of Favourite Newspapers

Chongolo Ashuhudia Wananchi wa Chamdindi Wakipata Maji Safi

0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata taarifa ya mradi wa maji Isimani Kilolo wenye thamani ya bilioni 9.2 ambao utahudumia vijiji 29 kutoka kwa Meneja  wa Mradi wa maji Isimani Kilolo Mhandisi Fabian Maganga  katika Kijiji cha Chamdindi, Jimbo la Isimani mkoani Iringa.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimtwisha ndoo ya maji Bi,Rosemary Zakaria Madulu (kushoto) mara baada ya kutembelea  mradi wa maji Isimani Kilolo wenye thamani ya bilioni 9.2 ambao utahudumia vijiji 29 katika Kijiji cha Chamdindi, Jimbo la Isimani mkoani Iringa.

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo  yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku saba kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuhamasisha uhai wa Chama ngazi za mashina pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi, huku maagizo mbalimbali anayotoa yakiendelea kutekelezwa.

Katibu Mkuu huyo ameambatana na wajumbe wawili wa sekretarieti ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu.

 

Leave A Reply