The House of Favourite Newspapers

Chris Brown, Nia Guzman Wavutana Kuhusu Matunzo ya Binti Yao

Chris Brown na mama mtoto wake mwanamitindo, Nia Guzman,  wamefikishana  tena mahakamani kuhusu matunzo ya binti yao aitwaye Royalty.

Nia anadai kwamba Chris anayeingiza Dola 4,269,067 ambacho ni sawa na karibu Sh. bilioni moja, anastahili kuwa anatoa Dola 21,000 (Sh. mil. 48) kwa mwezi kwa matunzo ya  binti yao.

Chris hivi sasa analipa kiasi cha Dola 2,500 (Sh. mil. sita) kwa yaya wa kumtunza ambaye ni Nia mwenyewe.

Brown amesema atapigana kadiri awezavyo ili Nia asimfanye benki ya kujichotea fedha bure kama atakavyo.

Nia ambaye anasema huingiza Dola 400 (Sh. laki tisa) kila mwezi, anasema fedha hiyo haiwezi kusaidia kuongezea katika matunzo bora ya binti yake huyo.

Comments are closed.