The House of Favourite Newspapers

Christian Bella Kumtunuku Nani.. Ni Pam D au Gigy Money?

0

MKALI wa masauti, Mwanamuziki Christian Bella, Mei 6, mwaka huu anatarajia kumtunuku ‘Krauni’ msanii Pamela Daffa ‘Pam D’ au Gift Stanfod ‘Gigy Money’ kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, Dar kwa kudodosha bonge ya shoo.

Bella ambaye mara ya mwisho alifanya shoo ukumbini hapo mwaka 2015, amejipanga kuwapa mashabiki wake burudani ya kufa mtu sambamba na kumtunuku msanii Pam D au Gigy Money ‘Crown’ ya kufanya naye kolabo.

Pam D

Kwenye shoo hiyo Bella atakuwa kama jaji atakayemchagua msanii mmoja wa kumtunuku kwa ajili ya kufanya naye kolabo ya bonge la ngoma.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo amewataka mashabiki wa Gigy Money na Pam D kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuhakikisha msanii wanayempenda anavishwa ‘crown’ hiyo na Bella.

Gigy Money

“Bella atafanya shoo ambayo haijawahi kutokea kwa kiingilio cha shilingi 7,000 kwa kumvisha crown Gigy Money au Pam D. Wasanii wengine watakaosindikiza kwenye shoo hiyo ni MC Darada, Mshindi wa Wikienda Music Search ‘WMS’ Frank Mgogosi ‘Mgogosi Melody’ na wengine kibao.

Leave A Reply