The House of Favourite Newspapers

Chuchu Ataja Sababu Kuachana na Filamu

0

 

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans amesema sababu iliyomfanya kuachana na filamu ni kutokana na maslahi kiduchu yanayopatikana kwenye filamu hizo.

Amesema kwa sasa mastaa wengi wanasubiria kuitwa kwa ajili ya kwenda kurekodi tamthiliya.

Chuchu ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, soko la filamu za Kibongo kwa sasa limeshapoteza mwelekeo baada kukosa wasambazaji kama waliokuwa wakiwatumia siku za nyuma.

“Sasa hivi ukijaribu kuandaa filamu na kuisambaza unavyojua, unajikuta umepata bonge la hasara.

“Kwa hiyo sasa hivi tunachofanya mastaa wengi ni kusubiria uitwe kwenye tamthiliya zinazoandaliwa na makampuni ambayo nyingi ndiyo yanalipa vizuri na kutuweka mjini.

“Kwa hiyo sasa tunategemea bahati tu ya kuitwa kama huna bahati imekula kwako. Ulimwengu tulionao siyo wa kutengeneza filamu yako kama zamani na kutegemea uuze eti upate faida, kwa sasa hakuna ndiyo maana wengi tumeamua kuachana nazo,” alisema Chuchu.

 

Leave A Reply