The House of Favourite Newspapers

CHUCHU ATOA POVU MIMBA KUCHOROPOKA

Chu­chu Hans

MWIGIZAJI wa kit­ambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Chu­chu Hans ametoa povu baada ya kudaiwa kuwa alinasa ujauzito ukachoropoka akiwa nchi­ni Afrika Kusini na mzazi mwenzie ambaye ni staa wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Chuchu alisema anawashangaa wa­naomfuatilia kila kukicha. Alisema ni ajabu kuona watu wanamfuatilia kama ana mimba au la.

“Kila kukicha watu wanapenda ku­fuatilia mambo yangu na sijui ni kwa nini maana hata kama nikizaa watoto kumi na Ray, ni sawa kwa sababu ni mwanaume na ananipenda na kujali, kwa hiyo hata kama imetoka nitabeba tena hivi karibuni,” alisema Chuchu.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.