The House of Favourite Newspapers

Chuma Hiki Kinakuja Simba Kutoka Klabu ya ASKO Kara ya Togo

0
Kiungo mkabaji, Efoe Novon raia wa Togo

SIMBA bado iko sokoni na sasa imepanga kumshusha kiungo mkabaji, Efoe Novon raia wa Togo huku wakipanga kumtoa kwa mkopo straika wao raia wa Zambia, Moses Phiri.

Novon kwa sasa anaitumikia Klabu ya ASKO Kara ya kwao Togo, ambayo alijiungana nayo tangu Novemba Mosi, 2020, akitokea katika Klabu ya AS Togo Port.

Safu ya kiungo ukabaji kwa sasa Simba iko chini ya Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma ambaye ni ingizo jipya.

Msimu huu Simba itakuwa na mashindano mengi ambayo watashiriki kuanzia ligi kuu, Kombe la Shirikisho la Azam, Ligi ya Mabingwa Afrika, Super League na Kombe la Mapinduzi hivyo inahaha kuhakikisha inajenga kikosi imara cha watu wa kazi kazi.

Chanzo cha kuaminika kutoka Simba kimeliambia Championi Jumatano kuwa, muda wowote kuanzia sasa uongozi wa Simba unaweza kumalizana na mchezaji Phiri ili apishe usajili mpya wa kiungo mkabaji raia wa Togo, Novon ambaye anaonekana kuhitajika kwa ajili ya kukata umeme kwenye klabu hiyo.

“Tunalazimika sasa kuanza mazungumzo na Moses Phiri ili tuweze kumruhusu kwenda kwa mkopo na nafasi yake tupate kiungo mkabaji ili aweze kuja kusaidiana na Kanoute ambaye anaonekana anaweza kuelemewa majukumu zaidi kutokana na wingi wa mashindano yaliyopo mbele yetu.

“Tulimuongeza Fabrice Ngoma kwenye nafasi hiyo ila kimsingi yeye siyo mkata umeme wa moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa Lwanga (Thadeo) au Fraga jambo ambalo tunaona kuna haja ya kutafuta tena mchezaji wa aina hiyo kabla ya uhitaji zaidi kwenye nafasi hiyo kuongezeka,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

Stori na Musa Mateja

USIOMBE IKUKUTE! ALIYEHUKUMIWA MIAKA 30 JELA kwa KESI ya KUMBAKA BOSI WAKE, AFUNGUKA MAZITO.

Leave A Reply