The House of Favourite Newspapers

Coastal Yataja Siku Ya Kumtambulisha Ali Kiba

Msanii wa Bongo Fleva, Ally Saleh Kiba ‘Ali Kiba’.

UONGOZI wa Coastal Union ndani ya siku hizi mbili unatarajia kufanya utambulisho wa nguvu kwa nyota wake wapya wa kikosi hicho akiwemo msanii wa Bongo Fleva, Ally Saleh Kiba ‘Ali Kiba’ ili watu wajue kuwa Kiba si msanii wa kuimba pekee bali yupo pia kwenye masuala ya soka.

 

Coastal Union kwa sasa inaendelea na usajili wake na tayari imeshawanasa nyota kadhaa, lengo likiwa ni kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Hivi karibuni gazeti hili la Championi, liliripoti kuhusiana na ishu ya Ali Kiba kutua ndani ya kikosi cha Coastal Union baada ya mwenyewe kuridhia kutaka kuitumikia timu hiyo, kilichokuwa kikisubiriwa ni kusaini mkataba.

 

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Steven Mguto, amesema wanahitaji kujiandaa zaidi ndipo waweze kumtambulisha nyota wao huyo mpya.

 

“Unajua Ali Kiba ni mtu maarufu san kutokana na kazi yake ya muziki, hivyo usajili wake unahitaji kuwa wa wazi zaidi ili watu wajue kuwa si kwamba anaimba tu bali watambue hata kwenye masuala ya soka yuko vizuri na sisi Coastal tumeamua kumsajili.

 

“Hivyo ndani ya siku hizi mbili litafanyika zoezi la kutambulishwa kwake pamoja na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa ndani ya kikosi cha timu yetu kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu,” alisema Mguto.

Stori na Martha Mboma, Dar es Salaam | Championi Ijumaa

Comments are closed.