The House of Favourite Newspapers

COLLEGE BOX FESTIVAL YATIA FORA MBAGALA

 

Tamasha la School and College Box Festival linaloendeshwa  na makampuni ya Global Group chini mkurugenzi wake Eric Shigongo, limetia fora katika shule ya sekondari ya St. Anthony iliyopo Mbagala Sabasaba wilaya ya Temeke.

Tamasha hilo lililoibua vipaji vingi vilivyopo katika  shule hiyo, lilifanyika siku ya jumamosi iliyopita na kuhudhuriwa na mhamasishaji mashuhuri barani Afrika Bw.Eric Shigongo aliyeambatana na Najma Paul ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha Dadaz kinachoruka kupitia EATV, wengine ni msimamizi wa kituo cha radio ya mtandaoni ,+255Global Radio Bw. Borry Mbaraka ambapo wote walipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi na kuwahamasisha kwa masuala mbalimbali ikiwemo Elimu na kuthamini vipaji vyao.

Akizungumza mbele ya wanafunzi,  Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo, aliwataka vijana hao kushikilia ndoto zao kwa maisha yao yote, kwa kuwa mafanikio yao yanategemea ndoto zao, ambapo jopo la wanafunzi hao walionyesha kufurahia na semina hiyo ambayo ililenga kuwajenga kifikira na kuwakuza kimtizamo.

“watoto wangu niwaambie kitu kimoja, hakuna ndoto inayotimia bila kuifanyia kazi hivyo basi mnatakiwa kufanyia kazi kwa bidii ndoto zenu ili zitime “alisema shigongo.

Stori:Ammar Masimba

Comments are closed.