The House of Favourite Newspapers

COSTECH Waikubali Barua Waliyoiandikia Twaweza -Video

 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Amos Nungu.

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  Amos Nungu,  amekiri kuwa barua iliyosambaa mitandaoni kwenda taasisi ya utafiti ya Twaweza  ni yao.

Nungu aliyasema hayo leo ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu barua iliyotumwa na tume yake kwenda Twaweza ikiwataka kujieleza kwa kuendesha utafiti bila ya kibali cha tume yake.

Kiasi cha wiki mbili zilizopita, Twaweza ilifanya utafiti kuhusu hali ya siasa na wanasiasa nchini na kutoa matokeo yake.

 

Comments are closed.