The House of Favourite Newspapers

Cristiano Ronaldo Amchumbia Georgina Rodriguez!

NYOTA wa soka duniani,  Cristiano Ronaldo, anayekipiga na klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno amepata mchumba!  Vyombo vya habari vya Ureno vilipomuuliza rafiki wa kike wa mwanasoka huyo aitwaye Georgina Rodriguez, alijibu habari hizo ni kweli.

Hivi sasa mrembo huyo anadaiwa kuwa katika mchakato bab’kubwa wa kujaribia nguo mbalimbali za ndoa ambapo pia  ‘wanahangaika’ kupata pete za uhakika kwa ajili ya kufunga ndoa hivi karibuni.

Wawili hao walikutana jijini Madrid, Hispania, katika duka la mavazi na vikorokoro vya mapambizo la Cucci ambako Georgina alikuwa anafanya kazi.  Watu hao tayari wana mtoto wa kike, ikiwa ni pamoja na watoto wa Ronaldo aliopata na wanawake wengine, ambao ni  Cristiano Junior, mwenye umri wa miaka minane na mapacha Eva na Matteo.

Comments are closed.