The House of Favourite Newspapers

Cristiano Ronaldo Jr Ajiunga na Kikosi cha Watoto cha Juventus

Image result for ronaldo junior on juve

Cristiano Ronaldo Junior, mtoto wa mwanasoka nyota duniani, Ronaldo, anayeichezea Juventus, amejiunga na kikosi cha watoto walio chini ya umri wa miaka tisa cha klabu kwa ajili ya mafunzo ya soka yanayojulikana kama  Pulcini 2010.

Kwa mujibu wa  Calciomercato ambaye ni  ‘mshikaji’ wa Ronaldo, mtoto huyo alicheza na watoto wengine wa watu maarufu na alionyesha umahiri mkubwa.

Kituo hicho kilianzishwa, miongoni mwa malengo yake,  kuendeleza vipaji vya watoto ambao baba zao nao walikuwa nyota wa soka.

Image result for ronaldo junior on juve

Baba yake alijiunga na Juventus msimu huu baada ya kukaa kwa mafanikio makubwa na klabu ya Real Madrid.

Edwin Lindege | Global Publishers na Mtandao.

Comments are closed.