The House of Favourite Newspapers

FAIZA: Sikwenda Msibani, Mama Mkwe Alikuwa Hanipendi Kabisa – Video

MZAZI Mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amesema hakwenda kwenye msiba wa mama mkwe wake, Desderia Mbilinyi kwa madai kwamba enzi za uhai wake mama huyo hakuwahi kumpenda hivyo asingeweza kuwa mnafiki kwa kujifanya mwenye majonzi ilihali hamaanishi.

 

Faiza amefunguka hayo wakati akihojiwa na Global TV Online baada ya kutoonekana kwenye msiba wa mama mkwe wake aliyeagwa jana Jumanne, Agosti 28, 2018 katika Kanisa Katoliki lililopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na baadaye kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Mbeya kwa mazishi.

 

“Mwanangu Sasha ameniwakilisha, kila mtu akimuona Sasha pale mibani basi amemuona Faiza. Sikujisikia kwenda kwa mtu ambaye hakuwahi kunipenda, ningepata dhambi, unatakiwa uende sehemu ambapo hata mwenyewe ukifika unakuwa na majonzi na mapenzi, sihitaji kwenda sehemu ambapo nikifika, uhusika wangu unakuwa hauednani na pale, mama hakuwahi kunitamkia kama hanipendi, lakini kuna mtu anakuonyesha matendo tu.

 

“Sikumpigia Sugu kumpa pole kwa sababu mimi na yeye hatupo kwenye wakati mzuri kwa muda mrefu, na pengine kama haitatokea tukakaa tukayamaliza, basi tutaishi hivi kwa wakati wote wa maisha yetu uliyobakia….. Nachoweza kusema tu ninamtakia mama apumzike salama na Mwenyezi Mungu atusamehe sisi tuliyobaki duniani, ” amesema Faiza.

Edwin Lindege | Global Publishers.

FAIZA ”Mama Mkwe Wangu Alikuwa Hanipendi Hata Kidogo”

Comments are closed.