The House of Favourite Newspapers

CUF YALAANI KUENGULIWA KINYANG’ANYIRO UDIWANI UBUNGO

Mkurungezi  Mipango Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (Cuf) Wilaya ya Ubungo, Hamdan Ngurangwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari.

 

 

CHAMA cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Ubungo kimelaani na kupina mpango wa  kuenguliwa kwa mgombea wao wa udiwani, Abubakari Nyamguma,  isivyo halali katika uchaguzi wa kata ya Kimara unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Wilaya ya Ubungo wa chama hicho, Basihir Ally amedai kuwa baada ya kuenguliwa kwa jina la mgombea wao, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilimtangaza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupita bila kupingwa.

 

 

“Cuf tunalaani kilichofanyika, ni uonevu, hujuma na hatukutendewa haki katika taratibu na hoja zilizotumika kufikia maamuzi hayo ambayo kimsingi ni batili na ya kibabe kwani sababu ya pingamizi iliyotolewa na mgombea wa CCM hazikuwa za kweli na ni za kubuni.  Ilitushangaza kuona msimamizi msaidizi wa uchaguzi kukubali na kusema amejiridhisha kuwa mgombea wetu alikuwa na kosa la kiapo, jambo lisilo la kweli kabisa,” ameeleza.

 

Kwa upande wake Mkurungezi  Mipango Uchauzi wa Cuf  Wilaya ya Ubungo, Hamdan Ngurangwa, amesema kuwa wanamalizia taratibu za kisheria ili waweze kufungua kesi mahakamani kupinga hujuma walizofanyiwa.

Comments are closed.