The House of Favourite Newspapers

Cuf Yawashukuru Watanzania Kufuatia Uchaguzi Mdogo wa Madiwani

  aNaibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdull Kambaya, akizungumza na wanahabar

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimewashukuru Watanzania waliokipigia kura katika uchaguzi mdogo wa marudio ya  udiwani uliomalizika Januari 22 mwaka huu.

Hayo yemesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdull Kambaya, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na chaguzi hizo ambazo walikuwa na kata 14 walizosimamisha wagombea.

Alisema kuwa uchaguzi huo uligubikwa na matumizi mabaya ya raslimali za umma na vyombo vya dola ambavyo vilikiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda kata 19 kati ya 20 na wakati huohuo CUF ilingia katika uchaguzi huo ikiwa imekwishapoteza kata moja ya Kimwani ambayo aliyekuwa diwani wa kata hiyo aliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.

b

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Kambaya alisisitiza kwamba licha ya kata hiyo ya Kimwani kuweka mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kunadiwa na Sumaye na Lowassa, chama hicho  hakikuweza kushinda kwenye kata hiyo.

c

Baadhi ya wanachama wa CUF waliohudhuria mkuatano huo.

“Tunapenda tueleweke kwamba uchaguzi huu si tu umetuwezesha kupigiwa kura na Watanzania, lakini pia kwetu sisi tuliutumia kama fursa muhimu ya ujenzi wa chama chetu kwenye kata za uchaguzi,” alisema.

Pia alitoa wito kwa wananchi na wanachama wote wa CUF kuendelea kukijenga chama hicho kwa nguvu zote na kukilinda kutokana na ubaya unaofanywa pia dhidi ya vyama vingine vya upinzani.

NA DENIS MTIMA/GPL

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Comments are closed.