The House of Favourite Newspapers

DAKTARI AKAMATWA NA GARI LA WIZI LA SERIKALI – VIDEO

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika oparesheni mbalimbali ya kukamata magari ya wizi na mitandao ya wizi wa magari, linamshikilia Daktari Yusuf Mwaipopo (42) wa hospitali ya Ephraem ya Temeke jijini Dar baada ya kukutwa na gari la wizi Mikumi mkoani Morogoro.

 

Akizungumza na wanahabri leo Jumanne, Novemba 6, 2018 jijini Dar, Kaimu Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Liberatus Sabas amesema gari hilo ambalo ni mali ya Wizara ya Afya liliibiwa hilo liliibiwa maeneo ya Mbagala, Temeke jijini Dar kabla ya kukamatwa.

Kukamatwa kwa mtandandao wa wizi wa magari;

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 14 kwa tuhuma za wizi wa magari.Watuhumiwa hao wamekamatwa sehemu mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam na mikoa mingine wakiwa na magari 7, Bajaji  moja na pikipiki moja ya wizi vyote vimeibwa maeno mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.

Watuhumiwa hao ni;

Luckman Ramadhani (36),Ignasi Faustine (35), Ally Shaweji (30),Stephen Mwanzalima (43),Emmanuel Mabula (42), Dismas Mfoyi (32), Nyamuhanga Matiko (29), Freeman Paul (35), Ayubu Makame (41), Erasto Nyamboneke (35), Seleman Saidi (42), Dickson Mbembaji (32), Ally Rashidi (35), Robert Nassoro (46)

Magari yaliyokamatwa ni
T 162 BLW Toyota land Cruiser  MALI YA UWT-TANZANIA
STL 6434 Toyota Land Cruise  MALI YA WIZARA YA AFYA
T 855 DLE Toyota Harrier
T 199 DEU Toyota Noah
T 249 DLL Toyota IST
T 255 AJG Rav4  gari hii ILIIBIWA udsm IKIWA na namba T 271 dff
T 556 DJQ Toyota Allion
MC 854 BYY TVS Honda
MC 639 BYA Bajaji.

 

Tarehe 1-11-2018 saa nne na robo usiku. Polisi walitilia mashaka Pikipiki. wakafanikiwa kuwajeruhi wote watatu. Jeshi la Polisi limeshauri Magari ya Umma wayapark kwenye yard za Serikali. Polisi watachukua hatua kwa dereva ambaye hatalaza gari ya Serikali kwenye ofisi ya Serikali.

 

Aidha, Polisi wamesema Swala la Mashoga lilipofikia aulizwe aliyoanzisha Kampeni. Kuhusu Kesi ya Dewji MO waandishi wataitwa kama kutakuwa na kitu cha kuwaambia. Kuhusu Wema kukamatwa peke yake, amesema Kesi ipo Mahakamani ila kila mtu atakamatwa.

Comments are closed.