The House of Favourite Newspapers

Daktari Feki Akamatwa Muhimbili Akitaka Kuwatapeli Ndugu Wa Mgonjwa – Video

0
Mussa Mawa

Mkazi wa Dar es Salaam aliyejitambulisha jina la Mussa Mawa amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akijihusisha na vitendo vya kutapeli wananchi wanaopata huduma kwa kujifanya daktari.

Mkuu wa Idara ya Ulinzi Bw. Alfred Mwaluko amesema kuwa wana usalama walimbaini daktari huyo feki akiwa kwenye harakati za kuwatapeli wananchi wanaouguza ndugu yao aliyelazwa jengo la Mwaisela.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Bw. Aminiel Aligaesha ametoa rai kwa watu wote wanaojihusisha na kutapeli wananchi katika eneo la Hospitali kwamba kwa sasa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama.

Leave A Reply