The House of Favourite Newspapers

DARASSA; ACHA MANENO WEKA MUZIKI!

MKALI wa michano Shariff Thabeet ‘Darassa’ ni mwanamuziki anayekubalika. Ukisikiliza ngoma zake za Shida, Hasara Roho, Too Much na nyingine nyingi utagundua jamaa huyu ana uwezo mzuri wa kutunga mistari yenye kuwateka mashabiki.

 

Hata hivyo ni ukweli kwamba Darassa ‘amehustle’ sana kwenye gemu. Takribani miaka kumi na ‘ushee’ amekomaa na amekuja kutusua zaidi mwishoni mwa mwaka 2016, baada ya kutoa Wimbo wa Muziki.

 

Muziki uligeuka kuwa wimbo wa taifa kwa takribani nusu au robo tatu ya mwaka 2017. Kila kona ya nchi vijana na wazee waliuimba wimbo huo. Ningependa kumshauri kupitia baadhi ya mistari yake kwenye Wimbo wa Muziki, kama ifuatavyo;

 

USIPOTEMBEA UTABEBWA MGONGONI

Katika wimbo wako Darassa uliimba mistari hii, kwamba; “Usipotembea utabebwa mgongoni!” Ni kweli kabisa. Inawezekana ulikuwa ukiwaimbia watu wengine lakini hata wewe mwenyewe Darassa ikiwa huhitaji kushituka na kugundua kwamba umelala na kutembea, basi utabebwa mgongoni na wakali wenye njaa ya kutusua zaidi kwenye gemu.

 

WANAOOTA MAPEMBE WAONGEZE MKIA

Sipendi kuamini kwamba Darassa umeota mapembe tukuo-ngeze na mkia. Sasa uta-kuwa umeota mapembe kwa kipi? Mafanikio hayo tu uliyoyapata? Jitazame upya bro bado tunapenda kupata vitu vikali kutoka kwako.

 

SINA MANENO YA KWENYE KANGA, KAZI JUU YA KAZI YAANI BAMPA TU BAMPA

Si kweli Kwamba huna maneno ya kwenye kanga. Mashabiki wako ushawaangusha mpaka dakika hii maana hizo kazi bampa tu bampa hatuzioni! Sasa hapa uliimba kwa kujifurahisha au vipi? Hebu tuonyeshe

 

WATCH YOUR SELF, USIJE UKAJICONFUSE

Mistari hii ni kengelekwako bro. Maneno mengi yanasemwajuu yako, mara oooh unatumia madawa, ndiyo yanakupoteza na mengine mengi. Sipendi kuamini maana sijathibitisha, lakini waswahili walisema lisemwalo lipo. Sasa kwa hili; Watch your self, usije ukajiconfuse.

 

UNATAKA KUKIMBIA NA HAUNA BREKI, WHAT DO YOU EXPECT?

Ukimya wako wakati mwingine unanifanya niamini kwamba ulijaribu kukimbia wakati huna breki. Lakini nimekufuatilia muda mrefu, wewe ni jembe na una uwezo mzuri. Sasa hebu endelea kututhibitishia kwamba una breki na unajua unachokifanya.

ACHA MANENO WEKA MUZIKI

Mwisho kabisa Darassa; Acha maneno weka muziki. Hilo tu ndilo mashabiki wako wanahitaji kusikia kwa sasa. Ukitoa ngoma kali na kuendelea kutuburudisha utazidi kupasua miamba na kupasua anga. Maana kumbuka ukisinzia na fegi utachoma kibanda!

Comments are closed.