The House of Favourite Newspapers

DARASSA AIBUKA, AFUNGUKIA DAWA ZA KULEVYA

Shariff Thabeet ‘Darassa’

BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu huku tetesi zikisema ametopea kwenye matumizi ya dawa za kulevya, staa wa Hip Hop Bongo, Shariff Thabeet ‘Darassa’ ameibuka na kufungukia tetesi hizo kuwa hazina ukweli na zilimuumiza mno.

 

Akizungungumza na Risasi Jumamosi, Darassa aliyewahi kutikisa na Ngoma ya Muziki alisema kuwa, mara baada ya kuachia Muziki aliamua kukaa kimya kwa ajili ya kuwa karibu na familia baada ya kupata mtoto wa kike.

 

Alisema katika mambo yaliyomuumiza ni waliokuwa wakizusha kwamba amepotezwa na dawa za kulevya.

“Watu walikuwa wakiongea wanayojua wao. Ukweli nipo fiti, sijawahi kujihusisha na vitu kama hivyo. Ukimya wangu sasa hivi umefika mwisho na nimerudi rasmi,” alisema Darassa. Wiki hii Darassa alitarajia kuachia ngoma yake mpya ya Achia Njia.

Stori: Shamuma Awadhi

Comments are closed.