The House of Favourite Newspapers

Darassa: Mastaa Wafanye Muziki Waache Show Off

0

Mkali wa Hip Hop Bongo, Sharif Thabeet ‘Darassa’ amewachana wasanii wenzie kuwa wafanye muziki waachane na show off zisizokuwa na maana.

 

Akipiga stori mbili tatu na AMANI, staa huyo ambaye mpaka sasa bado anatamba na albamu yake ya Slave becomes a king, alisema siku hizi mastaa wanaupelekesha muziki vile wanavyotaka wanasahau kuwa hii fani yenye heshima yake.

Siku hizi baadhi ya wasanii wanaufanya muziki kama kitu cha utani, yaani wanaupelekesha vile wanavyotaka, mara leo utashangaa kuona umechanganywa sijui na mambo ya wanawake, mara magari ya kifahari, ilimradi tu.

 

“Sasa mimi nawaomba kama kweli wameamua kufanya muziki wafanye muziki na sio kuleta mambo ya show off zisizokuwa na maana na kama wameshindwa watuachie sisi tuufanye,” alisema Darassa.

STORI: MEMORISE RICHARD

Leave A Reply