The House of Favourite Newspapers

Dau la Arsenal kwa Zaha Lakataliwa

ARSENAL wameelezwa kuwa kama wanamtaka mshambuliaji wa Crystal Palace, Wilfred Zaha watoe kitita cha pauni milioni 80, lakini wenyewe wamepeleka pauni milioni 40.

Mshambuliaji huyo anataka kujiunga na Arsenal lakini timu yake imesema haiwezi kukubaliana na ukubwa wa dau la pauni milioni 40. Arsenal wamesema wanaweza kutoa fedha hizo kwa mchezaji huyo tena watalipa kwa miaka mitano.

 

Hata hivyo, kaka wa mchezaji huyo amesema kuwa mdogo wake amekuwa akisema kuwa anataka kujiunga na Arsenal na anaamini kuwa msimu huu anaweza kwenda huko. Palace tayari kwenye usajili huu wameshapata pigo baada ya kumuuza beki wao Wan-Bissaka ambaye amekwenda Man United.

‘MAHAKAMA’ YAIHUKUMU STARS KWA MATOKEO MABAYA AFCON!

Comments are closed.