The House of Favourite Newspapers

Davido Aachia Ngoma Mpya

MWANAMUZIKI nyota kutoka nchini Nigeria Davido ameachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Risky’. Katika wimbo huo, Davido amemshirikisha msanii kutoka Jamaica Popcaan.

 

Wimbo huo ni mwendelezo wa freestyle yake iliyokwenda hewani ‘Kilo kan mi’ katika kipindi cha radio
Hot 97, huko New York mnamo Februari mwaka huu ambapo alisema utakuwa wimbo wa kwanza kwenye albamu yake inayokuja ya Good Time.


Davido aliachia kipande cha video katika kurasa zake za mitandao ya kijamii juu ya ujio wa wimbo huyo.
‘Risky’ ni wimbo wa pili ya Davido kwa mwaka huu 2019 baada ya hit yake aliyomshirikisha Chris Brown iitwayo ‘Blow my mind’.

Comments are closed.