The House of Favourite Newspapers

Ruvu Shooting Yaichinja Azam Mabatini

RUVU Shooting ya Masau Bwire jana ilimkaribisha vibaya Abdallah Zalala, Pwani kocha mpya wa Azam, Aristica Cioaba baada ya kumuadabisha kwa kichapo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mabatini mjini hapa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza kocha huyo raia wa Romania anakaa kwenye benchi la Azam FC baada ya kutua nchini Jumapili Iliyopita kuchukua mikoba ya Mrundi, Ettiene Ndayiragije.

Ushindi Huo umeipaisha Ruvu hadi nafasi ya nne kwenye msimamo huku Azam FC wakishuka hadi nafasi ya saba.

Bao pekee la Ruvu lilifungwa na Moses Shaban dakika ya 68 kwa shuti kali lililombabatiza beki wa Azam, Daniel Amoah na kuzama wavuni.

Comments are closed.