The House of Favourite Newspapers

Siri ya Bata la Davina na Aunt Dubai Hii Hapa

STAA wa filamu za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ baada ya kuonekana akila bata za mwisho wa mwaka kule Dubai akiwa na Aunt Ezekiel, amefichua siri kuwa kujiachia huko kumetokana na faida ya Vikoba vyao ambavyo wamejiwekea hisa kwa siku nyingi.

 

Akipiga stori na Showbiz kwa njia ya mtandao wa WhatsApp, Davina alisema watu wasishtuke sana kwa bata hizo kwani Vikoba vyao vina mpango wa kuwapeleka wanachama wake sehemu mbalimbali duniani hivyo wao bata lao wamekwenda kulila Dubai.

 

“Unajua watu wakituona tunakula bata kama hizi wanakimbilia kudhani tumewezeshwa na wanaume, hapana! Na hii naipigia mstari kwa sababu naujua ukweli, sisi tunawezeshwa na mfuko wetu wa Vikoba ambao una maendeleo makubwa na kwa mwaka huu watu wategemee makubwa kwani tuna filamu ambayo tutaicheza pia,” alisema Davina.

 

Davina alifunguka yote hayo baada ya kubanwa kuwa, inadaiwa safari yake ya Dubai nyuma yake kuna pedeshee, jambo lililomfanya aamue kuanika ukweli huo.

HAMIDA HASSAN | IJUMAA WIKIENDA

EXCLUSIVE: DJ wa ALIKIBA Afunguka Anavyofanya Nae Kazi!

Comments are closed.