The House of Favourite Newspapers

Dayna Abadilishwa na Tuzo

0

 

Na Boniphace Ngumije| UWAZI | SHOWBIZ

MWANADADA kiwango kwenye Tasnia ya Muziki Bongo, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amesema kuwa kubeba tuzo mbili za Bae kutoka nchini Nigeria katika kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kike Mwenye Sauti Nzuri ya Kutumbuiza (Best Vocal Perfomance Female) na Mwanamuziki Bora wa Kike Tanzania (Best African Artiste) kumembadilisha kwa kiasi kikubwa hasa katika utendaji wake wa kazi za muziki.

Akipiga stori na Showbiz, Dayna alisema kubadilika huko ni pamoja na kuongeza zaidi ubunifu katika kazi zake na kuongeza muda wa kufanya mazoezi maana kupitia tuzo hizo anategemea kupata fursa mbalimbali ikiwa na kumkutanisha na wasanii wakubwa toka nje.

“Kiukweli tuzo zimenibadilisha, zimenifanya niongeze ubize zaidi kwenye kazi zangu maana fursa pia zimeongezeka sasa ni lazima niwe fiti hasa nikikutana na wasanii wakubwa kutoka nje ninaotegemea kufanya nao kazi Mungu akijalia,” alisema Dayna.

Leave A Reply