The House of Favourite Newspapers

DAYNA AELEZA ALIVYOKUTANA NA WIZKID NIGERIA

Dayna Nyange.

WIKI chache baada ya kurejea Bongo akitokea Nigeria, mkali wa Ngoma ya Mafungu ya Nyanya akiwa na Marlow, Mwanaisha Said ‘Dayna’ ameeleza jinsi alivyokutana na mkali wa muziki nchini humo, Wizkid. 

 

Akifunguka mbele ya Star Showbiz, Dayna anayebamba kwa sasa na Ngoma ya Salama alisema kuwa, alipokuwa nchini humo alipokelewa vizuri na hata sapoti kubwa aliipata kutoka kwa Wizkid.

 

“Siwezi kusema kuwa nipo njiani kutoa naye wimbo, hiyo inabaki kimenejimenti kwa sasa lakini ninachotaka kushea na nyinyi, jamaa (Wizkid) ameweka heshima ya aina yake kwao, amekuwa ni mtu wa watu na hata nilivyokutana naye kila mmoja alikuwa akijiuliza huyu nani ametoka wapi, kumbe ni Mbongo mimi, haaa haaa,” alisema Dayna na kuongeza;

 

“Mbali na kukutana naye na kuzungumza naye mawili matatu, nilibahatika kutembelea redio zao, yaani karibu kila redio ni kama wameweka kautamaduni kao, kuna picha kubwa za wasanii wao wanaoiwakilisha nchi, kuna P Square, Wizkid, Davido, Yemi na wengine wengi tofauti na hapa Bongo kikubwa utakutana na saini za wanamuziki tu,” alimaliza Dayna

STAR SHOWBIZ

Comments are closed.