The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: Mtoto wa MAJUTO Afunguka Kumfukuza Mama Yao – VIDEO

KUFUATIA vuta nikuvute inayoendelea kati ya watoto wakubwa wa Aliyekuwa muigizaji nguli wa filamu Marehemu King Majuto, na Mjane wa marehemu Bi Aisha ambapo watoto hao wanadaiwa kumfukuza mama yao huyo kabla hata ya arobaini, Global TV imezungumza na mmoja kati ya Watoto hao anayeitwa Hamza Majuto.

 

Hamza ambaye siku chache kabla ya kifo cha Baba yake aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo amesema kuwa kwa sasa si busara sana kuzungumzia suala hilo kwani hata Arobaini haijafika ila anachojua Mzee Majuto hakuwa na mali sana zinazoweza kusababisha mgogoro katika familia aliyoiacha.

 

Fuatilia mahojiano haya mwanzo hadi mwisho ujue mbivu na mbichi kuhusiana na kinachoendelea kwenye familia ya Marehemu Majuto.

MTOTO “Mzee Majuto Hakuwa na Mali, Kaburi Litauzwa”

Comments are closed.