The House of Favourite Newspapers

Dayna: Nimehenya kutoa video

  MWANADADA anayefanya vizuri kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva kwa sasa na video yake mpya iitwayo Komela aliyomshirikisha Bill Nas, Dayna Nyange amefunguka namna alivyohenya mpaka kuikamilisha.

Akichonga na Gazeti la Amani, Dayna alifunguka kuwa changamoto kubwa iliyomkwamisha ni kukosa fedha kwani hana menejimenti ya kumsimamia.

“Nimehenya sana mpaka kuikamilisha video hii, unajua wimbo niliutoa tangu mwaka jana lakini mpaka mwaka huu nilikuwa bado sijatoa video, ilikuwa ni kwa sababu sikuwa na mkwanja,” alisema Dayna.

Comments are closed.