The House of Favourite Newspapers

Dayna nyange: Ni kigogo gani wa kuniweka mjini?

0

Dayna-nyangeWIKI hii tunaye msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Dayna Nyange anayetamba na Wimbo wa Angejua. Yupo hapa kujibu maswali 10 aliyoulizwa na Mwandishi Wetu Gabriel Ng’osha. Fuatilia…

Ijumaa: Shabiki wako angependa kwanza kujua maisha yako ya kimapenzi yakoje?

Dayna: Mimi ni mama wa mtoto mmoja, bado sijaolewa.

Ijumaa: Hujaolewa ina maana una mchumba, mpenzi au upoupo tu?

Dayna: Ninaye mpenzi ambaye siku Mungu akipenda huenda tukawa mwili mmoja.

Ijumaa: Unamaanisha yule uliyezaa naye au mwingine?

Dayna: Niliyezaa naye niliachana naye kitambo, ninaye mwingine ambaye tunapendana kwa dhati.

Ijumaa: Kuna tetesi kuwa anayekuweka mjini ni kigogo mmoja wa serikalini, hilo likoje?

Dayna: Kama nilivyosema, nina mpenzi wangu, hivi ni kigogo gani wa kuniweka mjini jamani?

Ijumaa: Kwa hiyo unataka kusema anayekupa jeuri ya kula, kuvaa, kumsomesha mwanao ni huyo mpenzi wako au unamaanisha muziki unakulipa sana?

Dayna: Si haba nashukuru Mungu kwani kupitia muziki naweza kumsomesha mwanangu na kufanya mambo mengine ya kimaendeleo.

Ijumaa: Mbona inaonekana kama vile nyota yako haing’ari kihivyo kwenye gemu?

Dayna: Ni mtazamo wa watu kwani binafsi ni msanii wa kitambo sana wa kike, nimedumu na ninaona muziki wangu unapiga hatua.

Ijumaa: Wimbo wako wa Nivute Kwako ulifanya vizuri sana, unadhani unaweza kutoa wimbo mkali kama huo tena?

Dayna: Ni kweli Nivute Kwako ilifanya poa ila haikunipa mafanikio kivile lakini Angejua imefanya vyema zaidi. Wanaofuatilia muziki wa Bongo wanajua hilo.

Ijumaa: Changamoto gani unakumbana nazo kwenye gemu?

Dayna: Ni nyingi sana ila kikubwa ni kukomaa, wapo wanaojaribu kubana lakini si unajua Mungu akikupangia hakuna wa kuzuia, unapasua tu!

Ijumaa: Kwa jinsi unavyoona muziki wa Bongo ulivyo, unadhani unaweza kumruhusu mwanao akikua awe msanii?

Dayna: Hiyo ni mipango ya Mungu, kikubwa asome kwanza kisha kipi atafanya akili yake itamtuma.

Ijumaa: Umesema una mpenzi, hivi siku moja ukimfumania utachukua uamuzi gani?

Dayna: Namuamini sana, sidhani kama hilo linaweza kutokea. Ila kwa sababu siwezi kuusemea moyo wake, siku ikitokea nitajua uamuzi wa kuchukua kwa wakati huo.

Leave A Reply