The House of Favourite Newspapers

Hizi Hapa Mbinu Za Kukabiliana Na Maumivu Ya Mapenzi

Image result for HAPPY COUPLES

KARIBU jamvini mdau. Ni Jumatatu nyingine tumekutana kupeana maujanja ya mapenzi na maisha kwa jumla. Unachopaswa kujua ni kwamba kila kitu kinastahili kulindwa na penzi lako linahitaji zaidi ya ulinzi. Hata kama unaona mambo ni mubashara kwenye uhusiano wako, lakini ulinzi ni muhimu mno.

Kama mada ya leo inavyojieleza, nataka tuangalie mbinu za kukusaidia kukukabiliana na maumivu kwenye uhusiano wa mapenzi;

1: MSAMAHA

Hakuna jambo ambalo hutuliza fikra na hisia za mapenzi kama kukubali kumsamehe yule aliyekuudhi kabla hata hajakuomba msamaha na kuamua kusahau yote yaliyotokea. Yawezekana wengi mtasema haiwezekani. Inawezekana na wote

waliojaribu mbinu hii walifanikiwa. Lazima kila mmoja aelewe kwamba unapokasirika au kuumizwa, anayeteseka siyo yule aliyekusa-babishia maumivu bali ni wewe mwenyewe. Hasira au maumivu ya kimapenzi huwa kama moto mkali ambao huitafuna taratibu nafsi ya mhusika. Ukisamehe maana yake unaupa moyo na akili yako nafasi ya kupata sehemu ya kutulia na kuuzima moto ambao tayari ulishaanza kukolea ndani yako.

2: MAZINGIRA

Baada ya kuumizwa na mwandani wako, mbinu ya kubadilisha mazingira na marafiki husaidia sana kukupa nguvu ya kukabiliana na msongo unaoweza kukusababishia madhara makubwa.

Unaweza kubadilisha mazingira kwa kusafiri, kubadilisha mpangilio wa chumba chako cha kulala na kuondoa vitu vyote vinavyoweza kukukumbusha hisia chungu za maumivu. Taratibu utaona akili yako ikianza kusahau maumivu. Yawezekana pia kuwa mpenzi wako ulishamtambulisha kwa marafiki zako nao wakamuona kama sehemu ya familia. Ukiendelea kujumuika na marafiki hao, watakuwa wanakukumbusha hisia chungu zitakazoendelea kukuumiza.Image result for HAPPY COUPLES

3: JIKUBALI

Utafiti wa kisaikolojia umebaini kwamba baada ya kutendwa kimapenzi, watu wengi hujishusha thamani na kudhani huenda wana udhaifu fulani ndiyo maana wapenzi wao huwasaliti na kutoka kimapenzi na watu wengine.

Kama ni mwanamke, muda wote atashinda kwenye kioo akijikagua kama ana kasoro kwenye sura na mwonekano wake. Mwanaume vivyo hivyo, atashinda akijiuliza kuhusu uwezo wake wa kumfurahisha mwenza wake au uwezo wa kifedha.

Kuyabadili maumivu haya kuwa furaha, jitazame kwa jicho la tatu na kujiambia kuwa wewe ni mzuri, una umbo zuri, unajua kukidhi haja za mwenzako mkiwa faragha na kwamba huna kasoro yoyote. Jipe nafasi ya kushughulikia maisha yako ya baadaye na suala la mapenzi achana nalo kwa muda mpaka utakapokuwa umetulia.

4: MAWASILIANO

Unapokuwa na maumivu ndani ya moyo, jambo la busara ni kusitisha mawasiliano ya aina yoyote na yule aliyekusababishia maumivu hayo. Wengi hufikia hatua ya kubadili namba za simu.

Hata kama njia uliyokuwa unapita kwenda kwenye shughuli zako za kila siku ilikuwa inakufanya ukutane naye, badilisha njia na ratiba yako kwa jumla.Related image

5: PENGO

Kosa ambalo wengi hulifanya baada ya kutendwa na wapenzi wao, ni kukurupuka na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na watu wengine muda mfupi baada ya kuumizwa. Badala ya kupunguza maumivu, utajikuta ukiongeza ‘stress’ kwani huyo unayedhani atafaa kuziba pengo, anaweza kuwa na maovu kushinda  aliyekuumiza. Jipe nafasi ya kukaa mwenyewe na kufikiria maisha yako ya baadaye, amini kwamba maisha yanawezekana hata ukiwa peke yako, kubaliana na kilichotokea na jiambie kuwa hutaki kurudia makosa kwa kuanzisha uhusiano na mtu atakayeuchezea moyo wako.

6: ZAWADI

Huenda wengi wakashangaa kwamba inawezekanaje kujipa zawadi mwenyewe? Inawezekana. Tembelea duka linalouza zawadi za kimapenzi kama maua, kadi, midoli au chocolate na jichagulie unayoipenda. Jiambie kuwa hakuna anayekupenda zaidi ya jinsi unavyojipenda mwenyewe.

POLISI LAWAMANI TENA! WADAIWA KUMKATA MGUU OSTADH na KUCHUKUA MILIONI 7 -YULE ALIYESOTA JELA MIAKA10

 

 

Comments are closed.