The House of Favourite Newspapers

DC BUNDA AMPIGISHA MAGOTI AFISA MTENDAJI WA KATA

MKUU wa Wilaya, Lydia Bupilipili anadaiwa jana Oktoba 2, 2018 alimpigisha magoti Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chitengule, Deus Kuliga alipokuwa akitoa taarifa ya kwa nini baadhi ya watendaji wa vijiji walishindwa kuhudhuria kikaoni.

 

Ofisa Mtendaji huyo alionekana kuwatetea viongozi hao kuwa walichelewa kupata taarifa na ndipo DC Bipilipili alipomwamuru kupiga magoti kwa kuwa ofisa huyo ndio alikuwa na jukumu la kuwapa taarifa viongozi wake.

 

Kwa upande wake Kulinga alisema; “Taratibu za kazi zifuatwe na mimi nipo tayari kujiuzulu lakini sipo tayari kudhalilishwa kama hivi utadhani nimeiba au nimetumia mali ya Serikali vibaya, Rais aangalie hali kama hizi”

 

“Mimi nina miaka zaidi ya 50, watoto 9 na wajukuu, kitendo cha kupigishwa magoti mbele ya kundi la viongozi wenzangu kama mtoto wa darasa la pili ni kunidhalilisha na hadi sasa sipo sawa,” alisema Kulinga.

BREAKING: ACT waicharukia NECTA kufuta Matokeo Darasa la 7

Comments are closed.